- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Shirika la Reli Tanzania (TRC) kupitia mzimamizi wa masuala ya kijamii Bi. Joyce Ponela wamefanya utambulisho rasmi wa program ya urejesho wa hali za Maisha kwenye mradi wa SGR katika maeneo unayopita katika halmashauri ya wilaya ya Manyoni, kikao ambacho kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Manyoni Ndugu Charles Edward Fussi Pamoja na Maafisa maendeleo ya jamii, Afisa Kilimo, Afisa Mifugo, Afisa Ardhi na Maliasili, Afisa mipango na Meneja wa SIDO mkoa wa Singida Bi. Agnes Yesaya.
Akiwasilisha programu hiyo kwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Manyoni Ndugu Charles Edward Fussi, Bi. Joyce Ponela kutoka TRC alisema program hizo zinalenga kuhakikisha Maisha ya watu walioathirika na kupisha mradi wanapata hali nzuri za Maisha baada ya athari hizo, ambapo alifafanua kuwa lengo la kualika watui wa SIDO na VETA ni kuwajengea uwezo kwa waathirika kupitia wataalamu wa Halmashauri ambao ndio waratibu wa shughuli mbalimbali zitakazoendeshwa kwenye utekelezaji wwa mradi.
TRC wamefafanua kuwa Mikakati mitano inayolengwa Zaidi katika program hii ni Pamoja na Mafunzo kwa waathirika waliopitiwa na mradi kwenye masuala ya usimamizi wa fedha baada ya kulipwa fidia, Upatikanaji wa ardhi inayobadilishwa na mmiliki wa ardhi ambapo mkakati umewalenga waathirika kupata elimu ya urasimishaji wa maeneo ili kupata hati miliki ili maeneo mapya watakayopata yaweze kuwa na tija Zaidi.
Mkakati mwingine ni mpango wa matarayisho ya ardhi ili kuongeza tija ya uzalishaji kwenye kilimo, Uhamishaji wa mifungo na upatikanaji wa malisho na maji kwa wafugaji Pamoja na Ujasiriamali na Stadi za Maisha Pamoja na ufundi kwa waathirika wa maeneo ya biashara.
Akitoa maneno ya Shukrani, Halmashauri ya Manyoni Ndugu Charles Edward Fussi, alisema kuwa anafurahi kwa mradi wa reli kuwajali wananchi na hasa Serikali kupitia TRC kuona umuhimu wa kutoa elimu hiyo yenye mikakati ambayo ina lengo la kuleta tija kwenye maendeleo ya wananchi wanaopitiwa na mradi wa reli ya Kisasa na ameahidi kutoa ushirikiano katika hatua zote
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
Sanduku la Posta: S.L.P 60, Manyoni
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 712 028027
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.