- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
HALMASHAURI YA WILAYA YA MANYONI
TAARIFA YA KILIMO CHA KOROSHO
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ni miongoni mwa Halmashauri 7 za Mkoa wa Singida yenye hali ya hewa inayofaa kwa kilimo cha korosho kutokana na utafiti uliofanyika na watafiti wa kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa mazao ya kilimo Naliendele kwa kushirikiana na watafiti wa mazao ya Kilimo Kanda ya Kati.
Baada ya kupitia tafiti hizi Uongozi wa Halmashauri uliona uanzishe zao korosho kuwa zao Mkakati, ili liweze kuchochea kwa kasi kubwa ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa Wilaya hata Mkoa kwa ujumla.
Ilibainika wazi kuwa zao hili linaweza kuwa zao kubwa la Biashara katika Wilaya Manyoni na Mkoa wa Singida, linaweza kuvutia uwekezaji wa Viwanda katika Mkoa huu.
Uongozi Halmashauri ya Wilaya Manyoni uliamua kuanzisha kilimo cha pamoja (block farming) lenye ukubwa wa takribani ekari 12,000 ambapo wamiliki wa mashamba ni wakulima na Halmashauri inasimama kama msimamizi mkuu wa hatua zote za kilimo bora, ambapo shamba hili pia linatumika kama shamba la mfano kwa wakulima wengine pia ambao wako nje ya eneo la mradi huu wa shamba la pamoja (Block Farming)
Katika msimu wa kilimo 2017 Halmashuri ya wilaya ya Manyoni ililenga kulima ekari 1,382 ambapo ilipokea pembejeo za zao la korosho kutoka Bodi ya korosho kwa lengo la kuzalisha miche bora ya korosho na kuisambaza kwa wakulima. Idadi ya miche halisi iliyozalishwa na kusambazwa kwa wakulima ni 109,752.
Aidha, kutokana na mwamko wa wakulima Halmashauri ya Wilaya ilipokea miche 9,867 kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Miche iliyozalishwa ilisambazwa kwa wakulima katika maeneo mbali mbali ndani ya halmashauri ambapo katika Shamba la pamoja (Block farming) ilipelekwa miche 37,000 na miche mingine 82,119 ilipelekwa katika vijiji vingine ambavyo vipo katika halmashauri ya wilaya ya Manyoni.
Sababu kuu tatu zilizofanya Uongozi wa Halmashauri kuchagua zao la Korosho kuchagua zao la Korosho kuwa zao Mkakati la Wilaya ni hizi zifuatazo:-
Kutokana na sababu hizo Uongozi uliamua kutenga maeneo ambayo yataweza kuanzishwa shamba la Mfano ambalo litalimwa kama shamba la pamoja (Block farming) ili liwe shamba kuwafundishia wananchi na pia kiwe kichocheo kikubwa cha uchumi wa Halmashauri kuweka soko la korosho katika eneo moja kubwa na chanzo kikuu cha ushuru wa Halmashauri.
Mwanzo wa usafishaji wa mashamba katika shamba la pamoja la kilimo cha korosho
Tunamkumbuka sana Baba wa Taifa hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere ambaye alitumia muda wake mwingi kuanzisha mashamba ya Ushirika katika maeneo mbalimbali Tanania miaka ya 1970. Baba wa Taifa alikuwa na maono makubwa na alikuwa na uchú wa kuona Tanzania inapaa kwenda kwenye uchumi mkubwa, yawezekana wakati ule kizazi kilichokuwa na nguvu ya kushika uchumi hakikumuelewa vizuri.
Zipo faida nyingi za kuwa na shamba la pamoja, tunaweza kubainisha wazi faida nyingi za kuwa na mradi huu ikiwa ni pamoja na kuanzisha uchumi wa pamoja wenye nguvu kubwa ambayo hawezi kuianzisha mtu mmoja kwa haraka kiasi ambacho kitawanufaisha wananchi wengi kwa muda mfupi, kudhibiti kutokea kwa majangwa katika mikoa ya kanda ya kati, kuanzisha kilimo cha pamoja cha zao la korosho na kuanzisha shamba kubwa la kuzalisha mbegu bora za korosho kwa ajili ya kuzisambaza kwa wakulima wa Mkoa wa Singida na Mikoa mingine.
Aidha, kilimo hiki cha pamoja kina manufaa mengine makubwa ikwa ni pamoja na;
Ili shamba hili liweze kukua kwa haraka, Serikali iliamua kutoa eneo bure kwa wananchi wote wenye kukubaliana na lengo la Halmashauri kufanya zao la Korosho kuwa zao Mkakati. Ili wananchi hao waoneshe utayari wao wa kulima Korosho walihitajika kutoa Sh 20,000 kwa ekari moja kwenye Kitongoji husika kwa ajili ya maendeleo ya kitongoji hicho ambacho kilitunza ardí hii ya Serikali.
Katika msimu huu mwitikio uliongezeka na wananchi waliojitokeza kuunga mkono kilimo cha zao mkakati la Korosho waiongezeka, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa kushirikiana na wadau wa kilimo cha korosho ililenga kupanda korosho katika shamba la pamoja kufikia ekari 7,000.
Mandalizi ya ufyekaji na kuchoma 2018/2019
Kulikuwa na mahitaji ya mbegu ni kilo 5,000 kwa ajili ya kupanda shamba la masgati ekari 7,000 na kinangali ekari 5000 na pia kwa wakulima waliopo nje ya shamba la pamoja (block farming) vijiji na vitongoji 41 takribani ekari 13,000.
Pia Halmashauri iliomba sulfa ya unga kilo 3,000 na viatilifu vinginevya maji lita 5,000
Bodi ya korosho Tanzania imefungua tawi lake hapa Manyoni ambalo litahudumia Mikoa ya Singida, Tabora, Kigoma na Katavi. Tunaishukuru serikali ya awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa MHESHMIWA RAIS Dr. John Pombe Magufuli kwa kutuchagua sisi Manyoni kuwa makao makuu ya Tawi hilo kwa ajili ya kuhudumia mikoa tajwa hapo juu.
Aidha, Ufunguzi wa tawi hili umeongeza mwitikio wa wakulima kujiunga na kilimo hiki pamoja na kuhudumia pia mikorosho ya zamani.
A: Ukuzaji zao la Korosho
B: Kuboresha miundombinu kimkakati
Katika misimu ya 2017/2018 na 2018/2019, Jumla ya Sh 608,113,907 kati ya Sh 619,627,000 zilitumika katika maandalizi ya mashamba na kuhakikisha eneo lililokuwa tayari katika shamba la pamoja linapandwa korosho.
Kati ya Sh 619,627,000 wakulima (wananchi) walichangia sh 582,656,800 na Halmashauri iliongezea sh 36,970,000 kuhakikisha maandalizi ya shamba yanakamilika katika maandalizi ya misimu yote ya 2017/2018 na 2018/2019.
Tarehe 18/4/2019 kamati tendaji ya Halmashauri ilikutana na kamati ya maendeleo ya Kata ya Mkwese (WDC) kwa ajili ya kuwasilisha maombi ya eneo la kulima korosho kwenye vitongoji vya Stendi, Kinangali, Tambukareli,Miyomboni, Majengo na Mbuyuni.
Maazimio ya kikao cha tarehe 18/4/2019.
Tahere 11/05/2019 palifanyika mkutano kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manyoni kwa kuwashirikisha wadau wote wa korosho.Wakulima walitoa maoni yao ili kufanikisha zao la korosho kwenye Halmashauri yetu ya Manyoni na pia kwa waombaji wapya walipewa maelekezo kwa ajili ya msimu wa 2019/2020 na moja ya mambo muhimu tuliyokubaliana na wakulima ni
Kuna aina mbili za gharama ambazo ni gharama za kuomba shamba na gharama ya kusafisha shamba.
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
Sanduku la Posta: S.L.P 60, Manyoni
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 712 028027
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.