- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Afisa Tarafa Nkonko Ndg Yahaya Njiku ameendelea na Ziara yake katika Kata ya Chikola Wilayani Manyoni ambapo amegawa Vifaa vya Shule kwa Wanafunzi wahitaji katika Shule ya Sekondari Kizigo.
Shule ya Kizigo ni Moja ya shule iliyofanya Vizuri katika Matokeo ya Mtihani wa kidato cha Nne na Matokeo ya Upimaji Mtihani wa kidato cha Pili 2024.
Akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi hao Njiku amesema lengo la kugawa vifaa hivi ni kuwasaidia watoto wasiojiweza kupata mahitaji muhimu wakiwa shuleni hapo.
"Kazi yetu ni kuwasaidia mtimize malengo yenu kwa kuzidisha kusoma kwa bidii bila kupata changamoto ya vifaa" alisema.
Njiku amesisitiza kuwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameleta fedha nyingi za Miradi ya Maendeleo ikiwemo miradi ya Elimu hapo Kizigo "Tumepokea zaidi ya Tsh 69 Mil kwa ajili ya Ukarabati wa Miundombinu.
Nawapongeze kwa kufanya vizuri katika Mitihani yenu lakini hii iwe chachu yakufanya vizuri zaidi katika Mitihani inayokuja, elimu ni urithi pekee utakao komboa Familia zenu na kuleta ustawi katika jamii"
Katika Ziara hiyo Afisa Tarafa aliambatana na Diwani wa kata ya Chikola Mhe Onesmo Malugu ambapo alisisitiza Wanafunzi kuwa Wazalendo na kuwa na Nidhamu wakati wote wawapo shuleni lakini pia Uongozi wa kata Utaendelea kutoa Ushirikiano kwa Shule wakati wote.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.