- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Ndg.Pendo Uswege Mwakila Afisa Ardhi Wilaya ya Manyoni alipotembelea na kufanya kikao kazi na Uongozi wa kata ya Mkwese, ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero.
Sanjari na hilo pia amekabidhi madaftari 12 kwa Wenyeviti wa vitongoji, Katibu wa baraza, Katibu mwenezi wa kata CCM ili waweze kuorodhesha Migogoro na Changamoto zinazoikabili kata hiyo ya mkwese kwenye Masuala ya ardhi.
Pia Aliwakumbusha kuwa wao kama Halmashauri ya Serikali ya kijiji ndio wasimamizi wakuu wa ardhi yote iliyopo ndani ya kijiji Chao, na kwa maana hiyo wasiuze ardhi kwa wawekezaji au watu wengine bila kufuata taratibu na sheria ya ardhi Na. 5 ya mwaka 1999, kijiji mwisho kutoa ardhi ni ekari 50 nazo hizo lazima mwekezaji aandike barua kwa Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji, Mwenyekiti anaitisha halmashauri yake, na wazo Hilo kupeleka kwenye Mkutano mkuu wa kijiji, mkutano huo ndio unaamua mwekezaji apewa au asipewe.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.