- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Manyoni, limepitisha Bajeti shillingi billion 29 kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Kikao hicho cha Baraza la Madiwani cha kujadili Mapendekezo ya Rasimu ya Mpango wa Bajeti kimefanyika Februari 23, 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Jumanne Mlagaza amesema Bajeti hiyo imezingatia kutatua kero mbalimbali za Wananchi ambazo zinawakabili.
“Tunashukuru kikao kimekwenda salama, na kwa kauli moja Waheshimiwa Madiwani tumepitisha Bajeti ya bil 29 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na Mambo mengine ya Halmashauri. Bajeti imezingatia kutatua kero za Wananchi”
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti CCM Wilaya Mhe. Jumanne Makanda amewashauri Madiwani na Watumishi wa Umma kuwa na Ushirikiano na Muungano katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo pia kuwaeleza Wananchi umuhimu wa Miradi inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao.
“Niwapongeze sana kwa hili la kupitisha Bajeti 2024/2025 kazi iliyobaki nikusimamia kikamilifu bajeti pale itakapo kuwa imeidhinishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Fanyeni kazi kwa kushirikiana na waelezeni wananchi nini Serikali yao inafanya katika Maeneo yao"
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.