- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
BARAZA la Madiwani katika Halmashauri ya Manyoni, limemchagua diwani wa Kata ya Nkonko, Mhe. Ezekiel Samwel Ezekiel , kuwa Makamu Mwenyekiti mpya wa halmashauri hiyo, kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024, akichukua nafasi ya diwani wa Kata ya Heka, Haruna Chimanga.
Ezekiel aliyekuwa mgombea pekee, ameshinda kwa kura zote za ndiyo, kutoka kwa madiwani 25 wa halmashauri ya Manyoni, hivyo kupata ridhaa ya kuongoza nafasi hii kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Nafasi hiyo awali ilikuwa inaongozwa na diwani wa Kata ya Heka, Mhe. Haruna Chimanga, tangu mwaka 2020, kabla ya kumaliza muda wake na kumpisha Makamu Mwenyekiti mpya, ambaye ni diwani wa Kata ya Nkonko, Ezekiel.
“Kipekee ninakishukuru Chama Cha Mapinduzi, Mwenyekiti na Katibu, waheshimiwa madiwani wote kwa kuteua Jina langu kwenye Chama ili kugombea nafasi hii na niwashukuru tena Madiwani kwa kunipa kura zote, niwashukuru pia wakuu wa vitengo na divisheni, ahsanteni sana, naahidi kishirikiana nanyi kikamilifu ili kuhakikisha tunaleta maendeleo katika Halmashauri yetu. Alisema Mhe. Ezekiel
Makamu Mwenyekiti ameahidi kuwatumikia kwa haki bila ya ubaguzi madiwani na wananchi, kwa kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali, ameahidi kuipaisha Halmashauri ya Manyoni katika maendeleo yaliyokusudiwa, kulingana na mipango iliyoandaliwa.
Awali Mwenyekiti wa uchaguzi huo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni, Mhe. Jumanne Mlagaza, alimpongeza Makamu Mwenyekiti mpya, kwa kushinda nafasi hiyo, na kumtakia kila la heri katika majukumu yake mapya ya kuwatumikia wananchi.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri, alitumia nafasi hiyo kumshukuru aliyekuwa Makamu Mwenyekiti (Mhe. Haruna Chimanga), kwa utumishi wake uliotukuka kwa kipindi chote cha uongozi wake, kwa kumsaidia sana katika kutekeleza kazi za kila siku.
“Ulipokuwa msaidizi wangu, ulitumia nafasi yako vizuri na kwa kweli ulinisaidia sana, ahsante sana kwa busara zako, naomba uendelee kumsaidia Makamu Mwenyekiti mpya, pale atakapohitaji msaada wako,”alisema Mwenyekiti
Baraza hilo liliofanyika jana kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manyoni, pia lilichagua wajumbe wa kamati mbalimbali kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024, ikiwemo kamati ya Fedha, Elimu, Afya na Maji, Kamati ya maadili na ile ya Uchumi, Ujenzi na mazingira.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.