- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba leo tarehe 5 Aprili, 2023 amemaliza mgogoro wa eneo kitakapojengwa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kufikia maamuzi kwamba chuo hicho kujengwa katika eneo la Manyoni Makao makuu ya Wilaya.
Maamuzi hayo ameyatoa katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kuwakutanisha wenyeviti wa Halmashauri zote za Wilaya hiyo, Wabunge wa Manyoni, Madiwani wa Halmashauri ya Itigi na Manyoni, Kamati ya Siasa ya Wilaya na ya Mkoa na Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya na mkoa.
RC Serukamba alipitisha uamuzi wa Chuo hicho kujengewa katika eneo la Setelite Manyoni karibu na eneo la mnada baada ya kuwahoji Madiwani wa upande wa Manyoni na Itigi na kubaini kwamba hapakuwa na ushirikishwaji katika upatikanaji wa eneo lililopendekezwa mwanzoni ambalo ni Kintiku Lusilile.
Madiwani pamoja na Wabunge walilazimika kupiga kura ya wazi kwamba ili kuamua chuo hicho kujengewa wapi kati ya Kintinku, Lusilile au Manyoni Setalite ambapo kura 10 zilitaka kijengwe Lusilile, 4 zilitaka kijengwe Itigi na kura 32 zilitaka kijengwe Manyoni.
Aidha Serukamba alieleza kwamba eneo hilo lipo katikati hivyo ni rahisi kufikiwa na wananchi wa maeneo yote ya Wilaya hiyo,
"Maoni ya wengi ni Maoni ya Mungu kwa kuwa wengi wameona chuo hicho kijengwe Manyoni lazima tufanye hivyo ili kiweze kuwasaidia wananchi kutoka pande zote, na wote naomba tuweze kusimamia hili," Alisema Serukamba
Hata hivyo amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo kuhakikisha eneo hilo linapimwa na wakabidhiwe Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati kwa ajili ya kuanza hatua za Ujenzi.
Hata hivyo amewataka Viongozi wa Wilaya hiyo kuandaa ziara katika kata zilipotakiwa kujengwa chuo hicho na kuwaelimisha sababu za msingi za kuhamishwa ujenzi huo.
Awali Mkurugenzi wa VETA kanda ya Kati John Mwanja, alieleza sifa ya eneo linalotakiwa kujengwa chuo cha VETA kwamba lisiwe na migogoro, kusiwepo na fidia lisiwe chini ya ekari 20.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.