- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Kemirembe Lwota amepokea Mabomba kwaajili ya Mradi wa Maji wa Kintinku-Lusilile
Akizungumza wakati akipokea Mabomba hayo Mhe. Kemirembe Lwota amesema Jamii ya wana Manyoni tunaendelea kumshukuru Rais wetu wa awamu ya sita Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutupa fedha nyingi sana kwaajili ya miradi ya maendeleo ndani ya Wilaya yetu.
"Ukanda huu tunakwenda kumtua mama ndoo kichwani kwani maji yatapatikana kwa wingi yakiwa safi na salama". Alisisitiza Mhe Kemirembe
Pia tunamshukuru Mbunge Mhe. Dkt Pius Chaya kwa jitihada zake za kuwasemea wananchi wa Jimbo la Manyoni Mashariki na kuhakikisha changamoto zilizopo katika maeneo mbalimbali zinapatiwa ufumbuzi na Serikali.
Naye Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Dkt Pius Chaya alisema Shida ya Maji tarafa ya Kintinku ilikua kama wimbo lakini sasa vijiji 11 vinakwenda kupata maji kupitia mradi huu wa Kintinku-Lusilile.
"Naomba mkandarasi wetu kuwa na Speed ili mradi huu ukamilike kwa haraka lakini ukiwa na viwango vinavyostahili". Alisisitiza Mhe. Dkt Chaya
Kwa upande wake Joakim Kalikawe mwananchi wa kata ya Maweni amesema Tunaishukuru Serikali yetu ya awamu ya Sita ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani, Mbunge wetu Mhe. Dkt Pius chaya na Madiwani wetu
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.