- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Kemirembe Lwota akiwa na Kamati yake ya Usalama ametembelea na Kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Gereza la Wilaya ya Manyoni
Miradi hiyo ni pamoja na Kilimo cha mbogamboga na matunda, Ufugaji pamoja na Shughuli za Ujenzi lakini pia Huduma za Kiafya.
Sambamba na Hilo Mhe. Kemirembe amepata wasaa wakuzungumza na watumishi wa Jeshi hilo la magereza pamoja na Wafungwa na Mahabusu waliopo katika Taasisi hyo.
Mhe. Kemirembe ameahidi kuhakikisha anakamilisha uwepo wa Huduma ya upatikanaji wa maji katika gereza hilo ili shughuli za kilimo ziongezeke zaidi na miradi mingine inayotumia maji kuendelea.
" Kilimo kinachofanyika hapa kina tija sana, mnatupatia mbogamboga, matunda lishe bora kwa wananchi wetu, nimeanza kwa kuhakikisha kisima kimechimbwa sasa nitaendelea kusimamia Ukamilishaji wa hatua zinazofata ili uzalishaji uongezeke zaidi.
Pia Mhe. Kemirembe amewanunulia King'amuzi Gereza la wanawake Manyoni lakini pia ametoa zawadi ya vinywaji kwa Watumishi, wafungwa na Mahabusu wote.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.