- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Dkt Pius Chaya tar 04 aprili 2024 ameshiriki Iftari na mafundi mbalimbali ya wananchi jimboni humo ikiwa ni ishara ya upendo kwa wananchi hao na tukio la ukarimu katika mwezi mtukufu wa Ramadhan unaoendelea.
Iftar hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Kemirembe Lwota na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na viongozi wa dini
Iftari hiyo iliambatana na dua ya kumuombea Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassani afya njema, maisha marefu na mafanikio makubwa zaidi.
Iftari hii imefanyika katika Msikiti wa Ijumaa ulipo Manyoni mjini na takribani watu 600 walihudhuria sadaka hiyo ya iftari.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Kemirembe Lwota mgeni rasmi katika hafla hyo alisema..
Tuendelee kudumisha Amani, upendo na Mshikamano kwani hii ndio nguzo yetu, tukiwa na Amani na upendo na Mshikamano tutakua na Amani tutaishi vizuri katika Wilaya yetu"
Maisha mnayoishi kipindi hiki cha mfungo tuendelee kuyaishi miezi yote 12 ya mwaka kwani ni maisha matakatifu na yanapendeza sana.
Aidha katika Sadaka hiyo ya Iftar Mhe. Dkt Chaya (mb) amechangia Mabati 60 kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Bakwata, Mkuu wa Wilaya Tsh. 500,000/=, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Tsh. 300,000/= na Mkuu wa Gereza Manyoni Tsh. 250,000/=
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.