- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kauli hii imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh Peter Serukamba tarehe 30 Novemba 2022 alipokua akitembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kuona namna miradi hiyo inavyotekelezwa na hatua ilipofikia.
Mkuu wa mkoa wa Singida Mh Serukamba akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkurugenzi Hailmashauri ya Wilaya ya Manyoni
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ina jumla ya mradi wa madarasa 85 yanayojengwa ili kupunguza upungufu wa madarasa nakupunguza umbali kwa wanafunzi katika kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni zikiwemo kata za Makutopora ,Saranda,Muhalala na Mkwese ambazo hazikua na sekondari na kwasasa sekondari hizo zinategemea kufunguliwa januari 2023.
Hatua mbalimbali za ujenzi wa miradi hiyo
Mh Serukamba amesema “Nawapongeza kwa hatua ya ujenzi kwa madarasa haya hatua ni nzuri ninaomba Muhakikishe mnaongeza juhudi ili miradi hii ikamilike kwa wakati na ikiwa ina kiwango kinachotakiwa. Mkurugenzi weka watu kila mradi wawe wanafatilia miradi hii kila siku ili twende na kasi itakayotufanya tumalize kwa wakati.
Sio kila siku tuwe tunakuja kuangalia miradi ya ujenzi tuu malizeni mapema kama tulivyokubaliana tarehe 15 ili kwakua msimu huu ni wa kilimo watu wahamie kwenye kilimo. Alisisitiza Mh Serukamba.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.