- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Bi. Anastazia Tutuba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tar 04 June 2025 kwenye Kikao chake na Wataalamu pamoja na Watendaji wa Kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri.
" Suala la Mapato ni ajenda ya kudumu hivyo hakikisheni kila mmoja kwenye eneo lake anasimamia vema mapato Ili kuleta Maendeleo ya Taasisi pamoja na Halmashauri kwa Ujumla"
Sambamba na Hilo Bi. Anastazia Tutuba amewataka Watumishi kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kwani kufanya kazi kama Timu kunaleta matokeo chanya kwa Taasisi.
Kwa Upande wake Deodatus Kangu ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Utawala Rasilimali watu amechukua fursa hii kujitambulisha kama mtumishi mgeni kwenye taasisi na kuomba ushirikiano.
" Niko Tayari kufanya kazi nanyi kwa kufata Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma hivyo Ndugu zangu naomba ushirikiano wenu Ili twende sawa"
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.