• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara Kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Manyoni District Council
Manyoni District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • History
        • Orodha Viongozi
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
      • Mchoro wa Kiutawala
      • Picha Ya Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala & Utumishi
        • Majukumu ya Idara
        • Legal Seatings on Council's level
        • Department Information
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utawala wa Mazingira na Usafi
      • Ujenzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
      • Huduma Zetu
        • Afya
        • Elimu
        • Maji
        • Kilimo
        • Mifugo
        • Uvuvi
    • Kilimo cha Korosho
    • Msimu wa mashamba ya Korosho 2019/2020
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha Ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba Ya Picha
    • Matokeo ya Kidato cha Pili 2018

"HALMASHAURI ZA MKOA WA SINGIDA ZASHAURIWA KUFANYA MAKISIO SAHIHI YA MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI PAMOJA NA KUONGEZA MAPATO YA NDANI"

Imewekwa Mtandaoni mnamo: January 19th, 2023

Wakurugenzi  wa  Halmashauri ya  za Mkoa  wa Singida  wameshauriwa kufanya makisio sahihi ya mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na kuimarisha  ushirikishwaji  wa Wakuu wa Idara  na Vitengo katika ukusanyaji  wa  Mapato  ya ndani hatua itakayopelekea  ongezeko la mapato na  kuondokana na utegemezi kutoka Serikali  Kuu.


Wito huo umetolewa na Katibu Tawala Msaidizi  sehemu  ya Menejimenti na na ukaguzi  Mkoa  wa Singida Bw. Evodius Katare  Hivi karibuni  katika kikao cha kufunga tathimini ya  vyanzo vya mapato ya ndani  ya Halmashauri  za Mkoa  wa Singida jijini Dodoma.

Bw. Katare amesema baadhi ya halmashauri zinakusanya mapato madogo ukilinganisha na hali halisi ya  vyanzo vya mapato vilivyopo katika Halmashauri husika na kupelekea  upotevu wa mapato ambayo yangetumika kuleta maendeleo.

‘’Inasikitisha sana kuona Idara ndani ya Halmashauri  zinakusanya fedha ndogo ukilinganisha  na Mshahara ,posho, motisha  wanazopewa , unakuta Afisa aliyeaajiriwa  kwa kazi inayoleta mapato kwa mwaka mzima anakusanya  mapato kwa mwaka mzima Mil. 2 hii siyo Afya kabisa kwa Halmashauri’’ Amesema Katare.

Aidha aliongeza kwakuzitaka Idara zinazohusika na  ukusanyaji  wa  Mapato  kuwa makini na kujitoa  kwaajili ya kazi hizi  na kuwataka kufanya kazi kwa Moyo kuhakikisha hakuna upotevu wa mapato  na kuacha uvivu  unaopelekea kutojali ukusanyaji wa fedha za Serikali.


Bw. Rwakatare amewashauri  Wakurugenzi  kujifunza na kujifunza na kubadilishana uzoefu  kwa Halmashauri zilizofanya vizuri  katika ukusanyaji wa  Mapato ya ndani  ili kuibua vyanzo vipya vya mapato  pamoja na kuona namna bora ya kuongeza mapato katika Halmashauri husika.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini  Ofisi ya Rais-TAMISEMI  ambaye ni Mwenyekiti wa wa Timu ya Mkoa wa Singida Bi. Nteghenjwa Hosseah amewasema  kuwa ofisi ya TAMISEMI  katika zoezi hili wamegundua  kuna baadhi ya ushuru wanakusanya Halmashauri moja huku zingine zikiwa hazikusanyi , na kusema  umefika wakati kama Mkoa kuweka utaratibu wa Halmashauri zote kukusanya kwenye vyanzo vinavyofanana bila kuwa na utofauti.


Zoezi hili limetoa fursa kwa Wataalamu  wa Halmshauri za Mkoa wa Singida kupitia bajeti zao kwa kina , kuongeza wigo wa mapato , kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato na kuandaa bajeti yenye uhalisia.






Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWAAJILI YA SHUGHULI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA September 15, 2024
  • TANGAZO LA UUZAJI WA MASHAMBA YA KOROSHO MWAKA 2022/2023 July 04, 2022
  • FOMU YA MAOMBI YA MASHAMBA YA KOROSHO MWAKA 2022/2023 July 04, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 12, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KARIBUNI MJIPATIE VIWANJA KWA BEI NAFUU

    May 05, 2025
  • "KIKAO CHA PHC CHAFANYIKA"

    April 26, 2025
  • "Jimbo la Manyoni Mashariki kubadilishwa Jina"

    April 26, 2025
  • "UJUZI UTABADILISHA MAISHA YA WATANZANIA"

    March 23, 2025
  • Angalia zote

Video

Ngoma za asili Siku ya UKIMWI Duniani
video zingine

Kurasa za Karibu

  • About Manyoni
  • Completed Projects
  • Ongoing Projects
  • Primary Schools Students Registration (Prem)
  • Instagram

Tovuti Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • President's Office, Public Service Management
  • Singida Region
  • Necta
  • MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
  • Kupata Salary Slip

Fuatiliaji ya watembezi wa Kidunia

world map hits counter

Kihesabia Watembezi

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

    HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI

    Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI

    Simu: +255 26 2540136

    Namba ya Simu: +255 26 2540136

    Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera za Siri
    • Malalamiko
    • Maswali ya Mara Kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.