- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Leo tar 25 April 2025 Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imefanya kikao na wadau mbalimbali kuthibitisha taratibu zote za mchakato wa Jimbo la Manyoni Mashariki kubadilishwa jina na kuwa Jimbo la Manyoni
Akizungumza wakati wa Kikao hicho Mh. Dkt Zainab Abubakar Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi amesema
" Tulipokea barua ya Mapendezo ya kubadili jina la Jimbo kutoka Jimbo la Manyoni Mashariki na Kuwa Jimbo la Manyoni, moja ya utaratbu wa mchakato ni kuja kuongea na wajumbe wa eneo husika juu ya namna ya mchakato uliotumika kukubaliana hilo ndomana Leo tuko hapa"
Naye Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Ndg. Kailima Ramadhan amesema
"Tumekuja kujiridhisha kuwa mchakato wa kubadili jina la Jimbo la Manyoni Mashariki umefuata utaratibu wa vikao vyote kisheria kuanzia vikao vya Kamati mbalimbali vya Halmashauri, Baraza la Madiwani, Kamati ya ushauri ya Wilaya (DCC) na Kisha Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC)"
Kikao hiki kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Vincent Mashinji, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Jumanne Mlagaza, Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Anastazia Tutuba, Wajumbe kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini, wazee maarufu, waheshimiwa Madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wakuu wa Divisheni na Vitengo na Ithibati ya Wajumbe wa Kikao hicho ilikua ni ndio na Tume Huru ya Uchaguzi wataendelea na mchakato wa kupitisha mabadiliko hayo na mchakato utakapokamilika itatangaza rasmi mabadiliko hayo.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.