- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mhe. Jumanne Shabani Mlagaza amaeiongoza kamati hiyo ya Fedha, Uongozi na Mipango kukagua Miradi Mbalimbali iliyopatiwa Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Makuru, Ujenzi wa Soko Sukamahela, Ujenzi wa Vyoo shule ya Msingi Mbwasa, Ujenzi wa Zahanati Mbwasa, Ujenzi wa Hosteli Shule ya Sekondari Sasajila, Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa Shule ya Sekondari Nkonko, Kikundi cha Vijana Kijiji cha Ipanduka, Ujenzi wa vymba vya madarasa 4 shule ya Sekondari Isseke, Ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa Shule ya Sekondari Sanza na Ujenzi wa Kituo cha Afya Sanza.
Hatua za Ujenzi Kituo cha Afya Makuru
Hatua za ujenzi Soko la Kijiji Sukamahela
Ujenzi wa Zahanati Mbwasa
Mhe. Mlagaza amesema Miradi hii kwa Ujumla inaendelea vizuri na kwakweli mmesimamia vyema lakini naendelea kusisitiza viongozi kushirikiana kwa kila hatua za ujenzi, Na pia Fedha mnazopata hakikisheni mnazifanyia kazi zilizoainisha kwenye muongozo wa mapokezi ya fedha hizo na kama kutakua na haja ya kubadili matumizi ya fedha basi ufuatwe Muongozo na Taratibu za Fedha.
Ujenzi wa Hosteli Shule ya Sekondari Sasajila
Pia Viongozi hakikisheni Miradi inakamilika kwa haraka pindi tuu mnapopatiwa fedha hizo na wananchi wanajitolea ili kupunguza garama za vitu ambavyo jamii wanaweza kushiriki shughili hizo ili miradi hii ikamilike kwa fedha mlizopatiwa.Alisisitiza Mhe Mlagaza.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.