- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Dkt Vincent Mashinji akiwa ameambatanana kamati ya usalama wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Miradi.
Ziara hiyo imefanyika leo 11, Disemba 2024 ambapo miradi mbalimbali imekaguliwa ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Shule ya Ufundi ya Sekondari Amali (Kintinku - Lusilile) ambapo amewataka wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati.
Kamati hiyo imekagua ujenzi wa shule mpya ya msingi umoja (Tambukareli), ujenzi wa miundombinu ya kidato cha tano Shule ya Sekondari Manyoni pamoja na Mradi wa Shule mpya ya sekondari Matori (Manyoni)
DC Vincent Mashinji ameelekeza kuwa miradi iyo ikamilike ndani ya Wakati ili ifikapo Tarehe 15, Januari 2025 shule zinapofunguliwa wanafunzi waweze kutumia madarasa hayo.
Kamati hiyo imekagua miradi inayotekelezwa katika jimbo la Manyoni na ziara iyo itaendelea kesho ambapo miradi inayotekelezwa katika jimbo la Manyoni Mashariki itakaguliwa
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.