- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamati ya Ushauri wa Kisheria Yatoa Msaada Manyoni: “Tuko Hapa Kwa Ajili ya Haki Zenu”
Manyoni, Singida – Wananchi wa Wilaya ya Manyoni wamepata fursa ya kipekee ya kupatiwa msaada wa kisheria kupitia Kliniki Maalum iliyoandaliwa na Kamati ya Ushauri wa Kisheria Mkoa wa Singida.
Akizungumza katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mecy Ngoi, ambaye pia ni Mkuu wa Mashtaka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Singida, aliwahakikishia wananchi kuwa Kamati hiyo ipo kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto zao kwa njia ya sheria.
> “Tumekuja kusikiliza kero na changamoto zenu, na tupo tayari kuwasimamia hadi mwisho ili mpate haki zenu. Msiogope, mueleze kwa uwazi," alisema Ngoi kwa msisitizo.
Naye Katibu wa Kamati hiyo, Bi. Maltida Meksoni, alitoa shukrani kwa Serikali kwa kuwezesha kamati hizo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, akieleza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha kila mwananchi anapata haki anayostahili kupitia usaidizi wa kisheria.
Kliniki hiyo ni sehemu ya jitihada endelevu za kuwafikia wananchi moja kwa moja na kuhakikisha mfumo wa haki unapatikana kwa wote bila ubaguzi.
@anastaziatutuba @drmashinjivincent @halimadendego @singidars @katibanasheria_ @ortamisemi @maelezonews
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.