- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kikao cha Kawaida cha Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kilichofanyika leo tarehe 20 machi 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.Kikao hiki kimeongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mhe. Jumanne Mlagaza kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Halmashauri.
Akizungumza kwenye kikao hiki Mhe Mlagaza amesema" Ni lazima tuwe wamoja katika kusimamia masuala ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na asipatikane mmoja miongoni mwetu anaetaka kupita njia yake Ili tufikie lengo la ukusanyaji tuliloweka
"Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Bi Anastazia Tutuba amesema"Bila kukusanya mapato hatuwezi kuwa na Fedha za kukamilisha miradi yetu, lakini pia hatutakua na Fedha za Asilimia kumi za kutosha kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu hivyo tushirikiane kwa pamoja Ili mambo yaende vizuri.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.