- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mafunzo kwa Viongozi (Wasimamizi na Wathibiti Ubora) wa Programu ya IPOSA Mkoa wa Singida yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tarehe 14 machi 2025
IPOSA ni Mpango umeandaliwa na TEWW chini ya ufadhili wa KOICA na unakusudia kutatua mahitaji ya kielimu miongoni mwa vijana walio nje ya mfumo rasmi wa Elimu nchini
Mkoa wa Singida Halmashauri zilizoguswa na mradi huu ni Manyoni, Itigi,Singida, Iramba na Mkalama.
Lengo kuu la mpango huu ni Kuwa na vijana walioelimika, wenye maarifa, ujuzi na stadi za kuweza kuchangia kwa haraka katika maendeleo ya taifa na kuhimili ushindani.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Godwin Gondwe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Halima Dendego amesema
" Mafunzo haya mliyopata yakawafikie kundi lengwa kulingana na mradi unavoelekeza Ili kuhakikisha wananufaika na Elimu hii kama ilivokusudiwa Ili vijana waelimike, wapate maarifa, ujuzi na stadi waweze kuchangia kwa haraka Maendeleo ya Taifa letu.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.