- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kuelekea Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 09 disemba Watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Rahabu Mwagisa wamefanya usafi maeneo ya Hospitali ya Wilaya pamoja na Bomani.
Pamoja na Usafi Mhe Mwagisa ameongoza zoezi la Kupanda miti pamoja na kuchangia damu
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Rahabu Mwagisa Akipanda mti
"Niwaombe sana tuendelee na utaratibu huu wa kufanya usafi katika mazingira yetu kama tulivyojiwekea utaratibu wa kila wiki siku ya jumatano na jumamosi ya mwisho wa mwezi ili mazingira yetu yadumu katika usafi na yapendeze lakini pia tuwe na hulka ya kupanda miti kwenye maeneo yetu, miti ya vivuli lakini pia miti ya matunda ili tupate matunda tuwe na afya bora. Alisema Mhe Mwagisa
MATUKIO KWA PICHA.
Zoezi la Usafi likiendelea
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Manyoni Ndg fadhili Chimsala akifanya usafi.
Zoezi la Upandaji miti likiendelea
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.