- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WAKULIMA WA KOROSHO SASA KUNUFAIKA .pdfHalmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa mara ya kwanza imezindua mfumo wa mauzo ya zao la korosho kwa njia ya mnada ambapo utasaidia kuongeza pato la Serikali na kuongeza kipato kwa wakulima na kuinua uchumi wa wanamanyoni. Mnada huo umezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa .
Akizindua mnada huo Mwagisa amesema kuwa katika uuzaji wa zao hilo wananchi watauza kupitia mfumo wa ushirika ambapo watakusanya korosho ghafi kwenye maghala ya vyama vya msingi na chama kikuu na kwamba mnada huo ni fursa ya ongezeko la kiuchumi kwa Wilaya ya Manyoni lakini na kwa Serikali pia.
Mwagisa amesema kuwa Wilaya ya Manyoni kama ilivyo kwa Wilaya nyingine Mkoani Singida Imepata fursa ya kipekee ya kulima zao la korosho japo wananchi baadhi wanaamini kuwa korosho hustawi zaidi ukanda wa kusini mwa Tanzania lakini sivyo tumeendelea kuona korosho ikistawi kwa wingi Manyoni na sehemu nyingine ndani ya Mkoa.
Katika hatua nyingine Mwagisa amesisitiza wakulima kulipwa kwa wakati fedha zao Ili kuweza kuwa na hari ya kuendelea kuuza kwa kupitia mnada na kwa kufanya hivyo tutainua uchumi wetu na tutapata fedha na kuongeza pato la Wilaya na Halmshauri lakini pia mkulima atanufaika
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.