- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba ameyasema haya tarehe 06 machi 2023 alipokua wilayani Manyoni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwenye Mkutani wa kusikiliza kero na kuzitatua ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika wilaya zote za Mkoa wa Singida.
“Ninawaomba sana wananchi wa Manyoni mnaodai fidia Halmashauri muwe na subira kwakua mchakato wa serikali unaendelea kuhakikisha mnapata fidia zenu kwa maeneo yaliyochukuliwa na halmashauri ya wilaya ya manyoni kwaajili ya matumizi ya Huduma za jamii”.
Mhe. Serukamba amesema; Ninawaahidi kufatilia kwa karibu suala hili la fidia zenu na ninajua tayari barua ya kuomba msaada wa kusaidiwa kulipa na serikali kuu deni hili ambalo ni kubwa tayari ilishaandikwa na halmashauri na kupelekwa kwakua ilikua ni maagizo ya Waziri Mkuu nitafatilia tena na tena ili kuhakikisha mnapata haki zenu.
Sambamba na hilo Mhe. Serukamba amewataka wananchi kuendelea kuamini kuwa Serikali yao iko kazini kwa kuhakikisha amani inakuepo wakati wote na kwa wale wanaojihusisha na mauaji katika wilaya ya Manyoni hakika Serikali itawatia nguvuni.
“Jambo hili la Mauaji ya Kishirikina yanayoendelea naomba niwaahidi wananchi kuwa uwe ni Mchungaji, uwe Shekhe, uwe mganga, uwe kasisi, uwe nani naomba nichukue fursa hii kuwatangazia kuwa Serikali itawakamata na kuwafikisha kwenye mkono wa Sheria na kama huamini na unajihusisha subiri tutakapokukamata ndio utaamini”.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.