- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mnyoni Mhe. Kemirembe Lwota mgeni rasmi kwenye Hafla ya kufunga mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba yaliyofanyika tarehe 15 Novemba 2023 katika viwanja vya Jumbe Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
“Niwapongeze Wakufuni kwa kuwapa Mafunzo haya ya Awali ya Jeshi la Akiba lakini niwapongeze wazazi kwa kukubali na kuwaruhusu vijana hawa kujiunga na mafunzo haya yanayokwenda kuwasaidia ninyi kipekee lakini pia kusaidia jamii lakini vile vile niwashukuru wote kwakuacha shughuli zenu na kuja kushiriki hafla hii ya vijana hawa wanaomaliza mafuno yao leo hii.”
“Kipekee niwapongeze vijana 85 mnaomaliza mafunzo haya leo hii na Niwaase mkawe wazuri wa Amani kwa Taifa lenu, Mtapewa mafunzo ya kukamata sawa na Askari asie na cheo ili mkasimamie amani na haki katika jamii yetu, Mkatimize wajibu wenu wa kulinda watu na mali zaona msitumie vibaya mamlaka mliyopewa”.Amesisitiza Mhe. Kemirembe
Mhe. Kemirembe amesema “Tushiriiane kwa pamoja ii kuleta Amani ya Manyon yetu hii sio kazi ya jeshi la Polisi pekeyao au Jeshi la Akiba pekeyao hili ni jukumu letu sote wananchi wa Manyonni hivyo tushirikiane ili tuweze kuwa salama kwa maendeleo ya Manyoni yetu.”
“Wote tuliopo hapa leo Nawaasa kuwa Mabalozi wazuri kuelimisha na wengine kuchukua tahadhari juu ya Magonjwa ya mlipuko kwani katika Mkoa wa Singida imeripotiwa kuwepo kwa ugonnjwa wa kipindupindu, hivyo tuchukue tahadhari kwakuhkikisha maeneo yetu yanakua safi na kuhakikisha tunanawa mikoni kwa maji tiririka tunapotoka chooni ili kujikinga na Magonjwa haya ya Mlipuko.”
Naye Luteni Kanali Enock Wiliam Liwembe Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Manyoni Amesema; Vijana hawa wanaomaliza leo mafunzo haya ya jeshi la Akiba tumewafunza Utii, tabia njema, Ulinzi kwa taifa lao, Mafunzo ya Mapigano, Bidii kwenye Utendaji kazi, kupiga shabaha, Mafunzo ya majeshi jiran kama Usalama, Polisi, Zima moto na Uhamiaji.
Wanahitimu Askari wa Jeshi la Akiba 85 ikiwa wanawake 22 na wanaume 63 walioanza mafunzo haya tangu tarehe 03 Julay 2023 na yamedumu kwa takribni miezi mine na leo tarehe 15 Novemba wanahitimu wakiwa na ujuzi wa kutosha tayari kulitumikia Taifa lao.
Imetolewa na
Kitengo cha mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.