- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tarehe 21/11/2023
Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg. Jimson Mhagama ametembelea na kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ilipo ndani ya Halmshauri yake.
Katika ukaguzi huo ameambatana na Watalaalmu mbalimbali wa Halmashauri akiwepo Afisa Mipango Halmashauri, Afisa Elimu msingi, Mhandisi, Mganga Mkuu pamoja na Afisa Habari
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Uchimbaji kisima, Ujenzi wa miundombinu ya maji, Kichomea taka na Ujenzi wa wodi zahanati ya kijiji cha Ikasi unaogharimu Tsh. Milioni 112, Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na ofisi 1 kijiji cha Sanza unaogharimu Tsh. Milioni 71, Ukamilishaji wa kituo cha afya kijiji cha Ntope Tsh. Milioni 20, Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa kijiji cha Igwamadete Tsh. Milioni 60, pamoja Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na ofisi 1 kijiji cha Mpapa unaogharimu Tsh. milioni 51,
Aidha katika ukaguzi wa Miradi iyo Mkurugenzi amesema;
"Tufanye kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano ili miradi yetu iendee vizuri bila shida yoyote na ikamilike kwa wakati"
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.