- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ni miongoni mwa Halmashauri 26 zinazotarajia kutekeleza mradi wa KIZAZI HODARI. Mradi wa KIZAZI HODARI ni mradi unaofadhiliwa na USAID wenye lengo la Kuimarisha Afya, Ustawi na Ulinzi kwa Watoto wanaoishi katika mazingira Hatarishi (WWKMH) na Vijana wenye umri 0-17 ili kufikia malengo ya Dunia ya Kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa asilimia 95.
Kikao cha Uzinduzi wa Mradi huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kimefanyika leo tarehe 24 Novemba 2022 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Meneja Mradi kanda ya kati Ndg Issa Murshid amesema mradi huu unatarajia kunufaisha walengwa 1779 katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Aliongeza kwa kusema mradi huu unatekelezwa katika Mikoa 7 na Halmashauri 26 lakini pia imegawanywa katika Kanda mbili yani kanda ya Kati yenye makao makuu yake Dodoma na kanda ya Kaskazini makao yake yakiwa Arusha. Mikoa hiyo 7 ni Dodoma, Morogoro, Tanga, Arusha,Manyara, Kilimanjaro na Singida na Kwa mkoa wa Singida utatekelezwa katika Halmashauri ya Manyoni na Halmashauri za Ikungi, Iramba na Manispaa ya Singida.
Mradi huu kwa Mikoa yote saba (7) Utagarimu kiasi cha Dola za kimarekani zipatazo Milioni 27 Umefadhiliwa na Shirika la Maendeea ya Kimataifa la Marekani (USAID) na Kusimamiwa na kutekelezwa na Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na utatekelezwa ndani ya miaka mitano (5) yani kuanzia 2022 na kumalizika 2027.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hiki cha uzinduzi wa Mradi wa KIZAZI HODARI Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mh Jumanne Mlagaza alisema; Mradi huu wa KIZAZI HODARI tunauzindua leo katika Halmashauri yetu na sote tuliopo hapa sasa tuna wajibu wa kwenda kuusimamia kwa nafasi zetu ili kufikia lengo linalotarajiwa katika mradi huu.Ni matumaini yangu tutakwenda kufanya vizuri katika utekelezaji wa Mradi ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Mh Samia Suluhu Hassan.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.