- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota
akiwa kwenye Ziara ya Kusikiliza na Kutatua Kero za Wananchi Kata
ya Sasilo Wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida Tarehe 25 Machi 2024,
"Ninatoa Siku Kumi na Nne, Ondokeni Eneo la Mbuga ya Lusiga, kama
una nyumba, kama unashamba hakikisha ndani siku kumi na nne unaondoka unapisha eneo lililo tengwa na kijiji kwa ajili ya malisho ya Mifugo"
Sambamba na haya Mhe. Kemirembe amewataka Wananchi kuacha Kujichukulia Sheri Mkononi na badala yake wafate Utaratibu wa Kisheria la Sivyo Watafungwa.
"Acheni kujichukulia Sheria mkononi hili jambo sio nzuri kabisa
maana kitendo hiko kinasababisha uvunjifu wa amani na amani ikitowea
itatuhusu sisi sote, kwahiyo jambo la kwanza na la msingi ndugu zangu
Tuilinde Amani yetu, bila amani, bila utulivu hatuwezi kufanya Shughuli
za Maendeleo"
Pia Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota amewataka Wakulima Waache Kulima Kienyeji watumie Mbolea ili Mkulima Aweze kunufaika na Kilimo Chake
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.