- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Dkt Vincent Mashinji akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Halima Dendego wakati wa Maadhimisho ya Juma la Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo yaliyofanyika tarehe 01 Oktoba 2024 Kata ya Chikuyu Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
" Tengeni Bajeti za Kuhudumia Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo rasmi Ili kuwezesha na kuhakikisha wenye mahitaji ya Elimu hii kuipata, Lakini pia wekeni mikakati ya kudhibiti changamoto za Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo"
Sambamba na Hilo Mhe Dkt Mashinji amepongeza jitihada zinazofanywa na Idara ya Elimu Mkoa wa Singida kwa kuandaa Maadhimisho haya lakini pia kusimamia Elimu hii ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo kuendelea kuwepo na kusaidia wengi katika Mkoa wa Singida
" Tumepita Mabanda ya Maonesho tumeona namna Elimu hii ya watu wazima na Elimu nje ya Mfumo ilivyosaidia wengi katika Mkoa wetu wa Singida hivyo niwapongeze sana sana kwa Kazi nzuri "
Vile vile Dkt Mashinji amewahamasisha na kuwasisitiza Wananchi kushiriki zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2024
" Kupitia hadhara hii napenda kuwakumbusha na kuwasisitiza kushiriki zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kuanzia tarehe 11- 20 oktoba tutakua na zoezi la kujiorodhesha kwenye daftari la mpiga kura na tarehe 27 Novemba ndio Siku ya Uchaguzi, hivyo niwaombe sana wananchi wenye Sifa za kugombea na kupiga kura tushiriki mazoezi haya kikamilifu
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.