- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Kemirembe Lwota alipokua kwenye hafla ya Uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani leo tar 04 Aprili 2024 iliyofanyika kata ya Heka.
" Ninawaomba sana viongozi wa vyama hivi vya Ushirika pamoja na wataalamu wetu kuendelea kutoa elimu kwa wakulima wetu juu ya matumizi ya mfumo huu wa stakabadhi ghalani kwani ni kwa manufaa yao"
Mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo ambao serikali umeuanzisha ili mkulima apeleke mazao
yake ghalani lengo ni kuongeza thamani ya mazao na mkulima kupata bei inayoendana na jasho la uzalishaji. Alisisitiza Mhe Kemirembe
Wito wangu kwa wakulima ni kuhakikisha mnazingatia muongozo uliotolewa na serikali kuhusu mfumo huu na mfumo huu ni kwa manufaa yenu na utawasaidia kuboresha maisha yenu.
Lakini pia wito wangu kwa vyama vya ushirika na viongozi ni kuhakikisha mnasimamia mfumo huu kwa ufanisi na kuhakikisha wakulima wanalipwa fedha zao kwa wakati na mtatue malalamiko yoyote yanayojitokeza
Sambamba na hilo Mhe. Kemirembe ameendelea kusisitiza juu ya matumizi ya Mbolea kwenye Kilimo ili kuongeza uzalishaji.
"Ndugu zangu lazima tujue kuwa tunapaswa kuongeza uzalishaji katika kilimo chetu kwa kuhakikisha tunatumia mbolea ya kutosha wakati wa kulima"
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.