- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mhe. Jumanne S. Mlagaza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tar 23 Mei 2024 alipokua akifungua rasmi Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani kwa robo ya tatu 2023/2024 uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
"Tuendelee kuimarisha Usimamizi wa Fedha Ili Miradi inayotekelezwa iwe na thamani ya Fedha iliyotolewa.
Lakini pia Viongozi wote na wataalamu kila mmoja atimize wajibu wake kikamilifu kwa kushirikiana na waheshimiwa Madiwani katika kusimamia miradi na kuimarisha Ukusanyaji wa Mapato pamoja na Usimamizi wa Fedha kwa ustawi wa wananchi wa Halmashauri yetu na Taifa kwa Ujumla" Alisisitiza Mhe. Mlagaza
Kipekee kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya Manyoni ninamshukuru sana na Kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia Fedha nyingi kwa mwaka huu wa Fedha 2023/2024 kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri yetu.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.