- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mhe. Dkt. Vincent Mashinji Mkuu wa Wilaya ya Manyoni tarehe 21 Juni 2025 kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri wa Kodi Wilaya ya Manyoni kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.
"Tuendelee kukutana na wananchi kwa maana ya wafanyabiashara wetu kuwapa Elimu juu ya ulipaji wa Kodi hizi, Tuwe na vikao nao mara kwa mara kwa makundi tofauti tofauti ili Elimu ya ulipaji wa Kodi hizi iwafikie wananchi wote"
Naye Ndg Frank Sigareti Meneja TRA Wilaya amesema
Wafanyabiashara wengi wamezoea kulipa kodi tarehe za mwishoni, na wengine kutolipa kodi kwa wakati, hivyo tunaendelea kuwafikia walipakodi kwenye maeneo yao ya biashara ili kuwasisitiza kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka adhabu za kutolipa kodi kwa wakati
Hata hivyo Meneja TRA ndg Frank Sigareti katika Taarifa yake amesisitiza Taasisi za Umma kudai risiti kwa wakati pindi tuu wanapopewa Huduma na mzabuni, Kwani wazabuni wengi wameonekana kusubiri muda wa malipo ndipo watoe risiti kinyume na sheria, Risiti inatakiwa itolewe pindi tu huduma inapotolewa au malipo ya huduma yanapofanyika kitakacho anza mapema ndicho kitalazimisha risiti itolewe kwa muda huo huo.
"Wazabuni wanapoomba zabuni kwenye Mfumo wa NEST ni vema Taasisi zetu zikadai Nyaraka muhimu pindi wanapoingia Mkataba na Wazabuni kwa mfano; Tax clearance na Cheti cha usajili wa VAT hii inatusaidia sana katika ukusanyaji wa Kodi
Vile vile Wananchi wanapaswa kuhakikisha wanadai risiti za EFD pindi tuu wanaponunua bidhaa na wafanyabiashara kuacha tabia ya kutotoa risiti halali kwani wakibainika faini yake ni milioni mbili hadi Milioni nne (2,000,000-4,000,000)
Sambamba na hilo Meneja TRA Wilaya amesema Kodi ya Zuio ya Pango la Biashara anaetakiwa kulipa ni Mwenye Nyumba lakini namna ya kulipa analipa Mfanyabiashara.
Hii ikiwa na maana kuwa Mfanyabiashara anapaswa azuie asilimia 10 ya malipo ya Pango kwa mujibu wa Sheria Ili ailipe TRA.
Mwisho Ndg. Frank Sigareti Meneja TRA Wilaya ya Manyoni amewashukuru sana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi kwa Ushirikiano mkubwa wanaompatia katika kutimiza majukumu yake ya kukusanya Kodi ya Serikali yeye na Timu yake
"Namshukuru sana Mkurugenzi Manyoni na Mkurugenzi Itigi kwakweli wananipa ushirikiano mzuri sana hata kufanya utendaji wangu wa kazi kuwa rahisi, tuendelee hivyo hivyo Ili kujenga Manyoni yetu kwa pamoja".
###Pamoja Tunajenga Taifa Letu ###
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.