- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano Mhe. Maryprisca Mahundi (Mb) Jana tar 13 Mei 2024 kwenye ziara yake alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mnara wa Mawasiliano Igwamadete Kata ya Isseka Wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida
"Rais wetu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan anatupenda sana ameona namna tulikua tunapata shida watu wa ukanda huu katika Mawasiliano, sasa ametuletea mnara ambao unaenda kutatua tatizo la Mawasiliano Igwamadete na vijiji jirani hivyo Rai yangu kwenu ni kuhakikisha Miundombinu hii inatunzwa vizuri ili isiharibike tuendelee kupata Mawasiliano vizuri.
Mhe. Mahundi pia alisema "Mhe Rais amefanya mambo mengi sana katika sekta mbalimbali kama Elimu, Afya, Mawasiliano, Uchukuzi na sekta zingine hata sisi wote ni mashahidi hivyo tunapaswa kumshukuru sana Rais wetu na kuunga mkono juhudi zake na kuhakikisha 2025 anashinda kwa kishindo.
Sambamba na hili Mhe. Mahundi alisema "Mwaka huu tuna uchaguzi wa Serikali za mitaa na Mwakani uchaguzi mkuu tushiriki vizuri katika chaguzi hizi na kuhakikisha tunachagua viongozi Wazuri watakaotusaidia lakini tuendelee kukianini Chama cha Mapinduzi kwani chini ya Mwenyekiti wake Dkt Samia Suluhu Hassan mambo tunayaona".
Pia niwaombe wananchi kuhakiki anuani zetu za makazi Ili kurahisisha Mawasiliano yetu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota aliwashukuru wananchi kwa kuhudhuria mkutano huo na kwa burudani mbalimbali lakini pia Alimshukuru Mhe. Naibu Waziri wa Mawasiliano kwa kutenga muda wake kufika kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mnara huo.
Kwa Upande wake Dkt Pius Chaya Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki alishukuru pia Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuhakikisha wananchi wangu wa Jimbo la Manyoni Mashariki wanapata Mawasiliano vizuri
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.