- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Kemirembe Lwota Mgeni rasmi kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 machi 2023 Kiwilaya yaliyofanyika katika Kata ya Nkonko Halmashauri ya Wilaya ya Manyaoni.
"Jamii nawaomba sana kupinga ukatili kwa wanawake kwani jambo hili ni baya sana katika jamii, tutaendelea kuelimisha juu ya kupinga ukatili wa wanawake na kwa watakaoonekana wanafanya hivyo hatutasita kuwachukulia hatua stahiki. Mwanawake wanaweza sana hivyo tuwape fursa sawa na wanaume katika kutoa mawazo, maamuzi na kuongoza pia kwani tunaona viongozi wakubwa katika nchi hii ni wanawake na wanafanya vizuri sana katika kulitumikia taifa. Mfano Raisi wetu Mhe. Dtk Samia Suluhu Hassani tunaona namna anavyoendesha nchi na maendeleo makubwa tunapata.
"Leo ni siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani naomba siku hii ikawe chachu kwa jamii kumuheshimu mtoto wa kike kwa kuhakikisha inamlinda na anapata haki zake zote za msingi ikiwemo elimu , nafasi ya kufanya maamuzi, nafasi ya kuongoza, nafasi ya kusikilizwa na mengineyo kwenye jamii, Atakaebainika anafanya vitendo vya ukatili kwa wanawake hatua kali zitachukuliwa dhidi yake". Alisisitiza Mhe Kemirembe.
Mhe. Kemirembe amesema Kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu 2023 ni “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia” basi ikalete mabadiiko kweli kwenye jamii kwa kuleta usawa wa jinzi ya kike na jinsia ya kiume na niwaombe sana kuitumia vizuri mabadilko haya ya teknolojia kwa maslahi mapana na jamii yetu ya sasa na kizazi kijacho.
Maadhimisho haya ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kiwilaya katika Kata ya Nkonko pia yaliambatana na Burudani mbalimbali zilizotolewa na washiriki wa maadhimisho hayo kama vile mashairi, kwaya, Bongo fleva, Ngoma za asili lakini pia kulikua na mechi kirafiki ya mpira wa pete kati ya timu ya wanawake kutoka Nkonko na timu ya wanawake kutoka Sanza na Timu ya wanawake kutoka Nkonko iliibuka kidedea kwenye mechi hiyo ya kirafiki.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.