- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yalisemwa na Mhe. Jumanne Mlagaza Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Leo tarehe 14 Mei 2024 Kwenye Ziara yake Alipotembelea na Kukagua Miradi ya Maendeleo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
Miradi liyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi, Ukarabati wa Hospitali ya Wilaya, Ujenzi wa Bwalo Solya Sekondari ya Wasichana na Ujenzi wa Vyumba 3 vya Madarasa na Matundu 8 ya Vyoo vya Wanafunzi, Ujenzi wa Matundu 3 ya Vyoo vya Walimu, Ujenzi wa mabweni 2 Chikuyu Sekondari.
"Twendeni Tukafanye Kazi, Tukasimamie Miradi kwa Umakini wa Hali ya Juu kwa kutumia Miongozo tulio patiwa katika Ujenzi wa Majengo ya Serikali pia Kamati za Ujenzi pamoja na Viongozi wa Serikali ya Kijiji na Kata Tembeleeni Miradi Msiwaachie mafundi, Hakikisheni Ubora wa Vifaa Vinavyotumiaka Ili majengo tunayojenga yawe imara na yakamilike kwa wakati unaotakiwa, Alisema Mhe Jumanne Mlagaza
Pamoja na Hayo Mjumbe wa Kamati ya Fedha Mhe. Robert Chanzi aliomba Kamati za Ujenzi "TUONDOKE PAMOJA NA KWA UMOJA LAKINI SIO TUONDOKE KWA PAMOJA LAKINI SIO KWA UMOJA" Toeni taarifa Ya kila jambo linaloendelea katika Miradi yenu ili Maamuzi Mengine yasije kuleta Sitofahamu
Lakini pia Upande wake Mhe. Benjamin Kamoga mjumbe Ameomba wataalamu kuhakikisha wanatembelea Mara kwa Mara Miradi ya Ujenzi inayoendelea Wilayani Ili kuendelea kuhakikisha ubora wa miradi hiyo.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.