- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mgeni rasmi Ndg. Abubakari Kisuda Afsa Utamaduni Halmshauri ya Wilaya ya Manyoni akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni katika uzinduzi wa Filamu iitwayo Barua ya Marehemu kutoka kwa wasanii wa Manyoni Arts Group uliofanyika usiku wa jana tarehe 12 novemba 2023 katika ukumbi wa Maktaba Social Hall.
“Mmefanya jambo zuri la kuigwa kwa kutuita leo ili kuzindua kazi yenu mliyoiandaa kwa muda mrefu ili kuelimisha jamii kupitia sanaa, kama serikali tutaendelea kuunga mkono juhudu zenu mnazozionesha katika kazi hii ya sanaa kwa kuhakikisha vikundi vyote vya sanaa vinasajiliwa na inapotokea fursa mbalimbali tuweze kuvitumia lakini pia kuna mikopo inayotolewa kwa vikundi vya sanaa nayo pia mnufaike nayo ili kukuza vipaji vingi zaidi”
Niwapongeze wadau wetu wote waliosapoti kutengenezwa kwa filamu hii ya Barua ya Marehemu wakiwemo Tungucha Pharmacy, Sultani Bekary, Narumu Star Hotel, Padre Dino Pre and Primary, Ngassa Trader, Mritho Credit co. limited na wengineo, tunatambua mchango wenu katika sanaa na tunaomba msichoke kusapoti kazi hizi. Alisema Ndg. Kisuda
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.