- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mhe. Kemirembe Lwota Mkuu wa Wilaya ya Manyoni alipokua akifungua Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya watu na Makazi Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tarehe 03 Juni 2024 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri.
"Niwaombe sana sana sisi tulioitwa Leo hapa, wasingeweza kuita wananchi wote wa Manyoni lakini wameona sisi wachache kwa nafasi zetu tuwawakilishe hivyo basi Tusikilize kwa makini tutakayoelekezwa na tukawe Mabalozi wazuri wa Usambazaji na Utumiaji wa Matokeo haya ya Sensa ya watu na Makazi katika maeneo yetu"
Ni wajibu wetu sote Wana Manyoni kuhakikisha kwamba tunayapata matokeo haya na kuyatumia katika kupanga maendeleo yetu, Maendeleo ya Kata, Maendeleo ya Wilaya, Maendeleo ya Mkoa na maendeleo ya Familia zetu tuzitumie taarifa hizi hata kwa Maendeleo ya Taifa letu.
Aidha Ndg. Benedict Mugambi
Kaimu Meneger wa Mfumo wa Kijiografia (GIS) kwa niaba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali amewashukuru na kuwapongeza Viongozi na washiriki wote wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni kwa kuhudhuria mafunzo hayo yenye tija kubwa kwani kuelewa kwao kutawapa urahisi katika Mipango ya Maendeleo.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.