- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwan Kikwete, amesema Serikali itaendela kutatua changamoto ya upatikanaji wa Ajira kwa Vijana kwa kutoa Mafunzo ya Fani mbalimbali yatakayosaidia vijana kujiajiri wenyewe.
Waziri Kikwete alisema hayo Wilayani Manyoni tarehe 22 Machi, 2025 wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi RC Mission alipotembelea chuo hicho kujionea fani mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.
Kikwete amesema zipo njia mbili zilizoelekezwa katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana ambazo ni kupitia ajira rasmi zinazotangazwa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, lakini pia kwa vijana kujiajiri wenyewe baada ya kupata ujuzi katika vyuo vya ufundi.
Amesema kinachofanyika katika chuo hicho na vyuo vingine vya aina hiyo nchini, ni kutafsiri maono ya Mhe. Rais, ambayo yamefafanuliwa vyema katika dira ya Taifa ya 2002 hadi 2025 inayoelekeza vijana kuajiriwa katika sekta rasmi na zisizo rasmi zitakazowasaidia kubadilisha maisha yao lakini pia kukuza Uchumi wa taifa.
Naye Mkuu wa chuo hicho, amesema chuo hicho kilianzishwa kwa lengo la kutoa ujuzi kwa watu wenye ulemavu kulingana na aina ya ulemavu walionao, ili kuwawezesha kupata utaalam utakaowainua kiuchumi na hivyo kuwa na mchango katika maendeleo ya jamii.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.