- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe. Dkt Vincent Mashinji Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ameongoza Kikao cha Viongozi wa Dini na Wazee Maarufu kilichofanyika tarehe 24 Juni 2025 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Dkt Vincent Mashinji amewaomba Viongozi wa Dini kuendelea kuhamasisha waumini kuwa na Umoja kwani ni moja ya Tunu ya Taifa letu.
"Ninawaomba sana Viongozi wa Dini kuendelea kuwahubiria waumini kuwa na Umoja kwani Umoja huleta Amani na Utulivu kwenye Taifa letu hasa katika kipindi hiki kinachoendea Uchaguzi Mkuu Ili watu wawe na Utulivu na Amani"
Sambamba na hilo Dkt Mashinji amewasisitiza Viongozi wa Dini na Wazee Maarufu kuendelea kuimuunga mkono Serikali ya Awamu ya sita Chini ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Juhudi kubwa za Maendeleo katika Maeneo yetu na Tuliombee Taifa letu pamoja na Viongozi wetu"
Pia Dkt Mashinji amewafahamisha Viongozi wa Dini na Wazee Maarufu juu ya Maandalizi ya Mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Katika Wilaya ya Manyoni kuwa tarehe 24 Julai 2025 tutaupokea Mwenge wa Uhuru Katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na tarehe 25 Julai 2025 katika Halmashauri ya Itigi.
"Tunatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru Katika Wilaya yetu ya Manyoni tarehe 24 Julai 2025, na kama tunavyofahamu tuna Halmashauri mbili hivyo tarehe 24 Julai tutaukimbiza katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na tarehe 25 Julai katika Halmashauri ya Itigi hivyo Watangazieni waumini wenu kushiriki Mapokezi haya ya Mbio za Mwenge "
@ikulu_mawasiliano
@ortamisemi
@ofisi_ya_makamu_wa_rais
@owm_tz
@singidars
@halimadendego
@drmashinjivincent
@anastaziatutuba
@manyonidc
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.