- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. kemilembe Lwota Leo tarehe 08 machi 2023 alipokua akiongoza zoezi la Usafi lililoanzia Hospitali ya Wilaya ya Manyoni kuelekea maeneo yote kuzunguka Mji wa Manyoni.
"Usafi ni muhimu sana kwa afya zetu ili tuendelee kufanya shughuli za uzalishaji na maendeleo ya taifa hili, Hatuwezi kuwa na afya njema kama mazingira yetu ni machafu namna hii, Hivyo niwaombe wananchi wa Manyoni kata zote tuwe na desturi ya kufanya usafi kwenye maeneo yanayotuzunguka ili kuepuka magonjwa mbalimbali ya milipuko yanayosababishwa na mazingira kuwa machafu"
Lakini pia leo nimepita kuongoza hili zoezi la kufanya usafi kwa mara ya kwanza ninahamasisha lakini jumatano ijayo nitapita kukagua usafi ili kuhakikisha kila mmoja wetu amefanya usafi kuzunguka eneo linalomzunguka la kuishi au la kufanya biashara, kwa ambae atakua hajafanya usafi siku hiyo mpaka mimi napita atatoa faini ya shilingi elfu hamsini (50,000/=) na atalazimika kufanya usafi.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ndg Heri A. kaombwe amesema tutaendelea kuhakikisha tunaboresha na kuongeza vitendea kazi kwaajili ya Usafi kwa maeneo kama Hospitali na mengineyo ili kuhakikisha usafi unafanika kwa kiwango kizuri kinachoridhisha. na kuhakikisha watu wanaendeea kuhamasishwa kufanya usafi katika maeneo yote yanayowazunguka.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.