- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Kemirembe Lwota leo Tarehe 13 Disemba 2023 ameongoza watumishi wa Wilaya ya Manyoni pamoja na Wananchi wa Manyoni kufanya Usafi wa Mazingira kuzunguka maeneo yote ya Mji wa Manyoni.
"Ndugu zangu suala la Usafi ni muhimu na lazima kwani kwa kuzingatia usafi wa Mazingira tutaepuka Magonjwa ya milipuko hivyo niwaombe sana kuzingatia mazingira tunayoishi na yanayotuzunguka yanakua safi wakati wote" Alisema Mhe. Kemirembe
Sambamba na hilo Mhe Kemirembe amewataka wananchi kuzingatia ratiba ya Usafi na utaratibu uliowekwa wa kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka ikiwemo maeneo ya biashara zao kila Jumatano ya kila wiki na Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
"Utaratibu wetu ni kila Jumatano ya kila wiki usafi unafanyika na kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi nawaomba sana kuzingatia hilo na sitakubali kuona mtu anaendelea kufanya biashara wakati huo wa kufanya usafi na mazingira yake ni machafu nitamchukulia hatua stahiki"
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.