- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh Rahabu Mwagisa ametoa agizo hilo kwa Afsa Maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kuhakikisha anatembelea vikundi vya kina mama na vijana wajasiriamali wanaofanya biashara zao ndani ya Standi ya Wilaya ya Manyoni na kuvikagua kuhakikisha vikundi hivyo ili waweze kupatiwa Mikiopo ya Asilimia 10 inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri zote bila riba.
Mh Mwagisa ameyasema haya alipotembelea standi hiyo ya Manyoni tarehe 03 Novemba 2022 ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake. Sambamba na Hilo Mkuu wa Wilaya amewaahidi Wanachi kusimamia na kuhakikisha mazingira ya standi hiyo yanaboreshwa haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na Barabara kutengenezwa, Vyoo kuboreshwa, Wajasiriamali kupata vibanda, Taa kuwekwa na pia kuhakikisha Magari yote yanaingia standi na sio kupakia na kushusha nje ya standi.
Kina mama na Vijana Wajasiriamali Stand ya Manyoni.
Baada ya kuzungumza na Wajasiriamali standi ya Manyoni Mh Mwagisa alienda kufanya mkutano wake wa hadhara katika viwanja vya mnadani Majengo ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi hao.Moja ya kero iliyojitokeza sana kwa wakazi wa majengo ni Ardhi na Fidia kwa mradi unaoendelea wa SGR na wananchi walitatuliwa kero zao papo hapo kwakua wakuu wa Taasisi hizo walikuepo kwaajili ya kutatua kero hizo za wananchi.
Mh Mwagisa akizungumza na wananchi.
Wananchi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Manyoni Mh Jumanne Mankanda alipata fursa ya kuzungumza na wananchi na Kuahidi kuendelea kuisimamia na kuishauri Serikali ili kutatua kero za Wananchi na kuleta Maendeleo
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.