- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mafunzo haya yametolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muugaano wa Tanzania chini ya Wizara ya Elimu na Ofisi ya Raisi kupitia programu ya Shule Bora.Mafunzi haya yameanza tarehe 31 julai hadi tarehe 03 agosti 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Mafunzo hayo kwa niaba ya Afisa Elimu Mkoa Bi. Regina Yaghambe Amesema;Awali ya yote, napenda nimshukuru Mungu aliyetujalia uhai na kutuwezesha kuwepo hapa leo,Nipende pia kuishukuru Wizara ya Elimu na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kuandaa mafunzo haya ambayo yanaratibiwa na kufadhiliwa kupitia programu ya Shule Bora.
Niwashukuru pia ninyi washiriki kwa kufika na kwa namna ya pekee niwashukuru sana wawezeshaji wetu kwa kukubali kuleta mafunzo haya katika Mkoa wetu wa Singida, Pia niwashukuru wafanya kazi wa programu ya Shule Bora kwa kuendelea kushirikiana nasi katika masuala yote ya Elimu katika Mkoa wetu. Alisema Bi.Regina
Bi.Regina Yaghambe Alisema Mafunzo haya yanayohusu Elimu jumuishi ni muhimu sana kwa sababu yanatujenga sisi watendaji kufahamu mbinu bora za kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi wa makundi yote kumi na matatu (13) kama yanavyotambuliwa na Mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi wa Mwaka 2021/22 hadi 2025/26.Ni Dhahiri kwamba madarasa yetu yana wanafunzi wenye mahitaji tofauti ya ujifunzaji, na wote wanatakiwa wapate elimu bora.
Mafunzo haya yatawajengea washiriki ambao ni walimu uwezo wa kutumia mbinu za ufundishaji na ujifunzaji jumuishi ili kuleta matokeo chanya ya ujifunzaji kwa wanafunzi wote kwa kuzingatia mahitaji yao na viongozi wa elimu watawezeshwa namna bora ya kusimamia na kuratibu mafunzo haya ili yafanyike katika jumuia za Ujifunzaji (JzK) katika kila shule na hivyo kuwafikia walimu wote katika shule zote zenye wawakilishi hapa.Alisisitiza Bi. Regina
Ni matumaini yangu kwamba kama kila mmoja wetu atasimama katika nafasi yake, tutakuwa katika nafasi nzuri ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi wote, na kwa kufanya hivyo tutapata matokeo chanya na tutakuza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika mkoa wetu.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.