- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Haya yamesemwa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl Dorothy Mwaluko tarehe 31 Januari 2023 Alipokua akifungua Mkutano wa Uhamasishaji wa Programu ya Shule Bora kwa Wasimamizi wa vyombo vya Habari na Wahariri Mkoa wa Singida Uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
“Waandishi wa habari wa Mkoa wa Singida Mnatakiwa muwe wazalendo kwa Kuandika habari nyingi za Maendeleo ili kutangaza Mkoa wet una sio kukimbilia kuandika zile zinazohusu mabaya tuu japo hazikatazwi”.
Aidha Mwl Mwaluko aliwataka waandishi kwenda vijijini kuandika habari za uchunguzi ambazo zitasaidia kuibua changamoto za wananchi,watumishi wa kada zote pamoja na miundo mbinu mbalimbali ili ziweze kufahamika na kutafutiwa ufumbuzi kwa haraka iwezekanavyo.
Sambamba na hayo Mwl Mwaluko alitumia nafasi hiyo kuwaeleza wana habari hao kuwa mwaka huu Mkoa wa Singida tunatarajia kufanya maadhimisho ya Miaka 60 tangu uanzishwe mwaka 1963 hivyo aliwaomba waandishi wa habari waandike habari mbalimbali zinazohusu Mkoa wa Singida ili kuutangaza Mkoa huu kuelekea Kilele cha Maadhimisho hayo yatakayofanyika oktoba Mwaka huu.
Meneja Mawasiliano wa Shule Bora Raymond Kanyambo akizungumzia program hiyo ya shule bora amesema ni priogramu ya Serikali inayofadhiliwa na UKAID wenye lengo la kukuza na kuboresha ufundishaji na ujifunzaji mashuleni ili kuboresha elimu na kuhakikisha Watoto wote wa kitanzania wa kike na wa kiume wanapata elimu bora.
“Programu hii ya miaka sita inatekelezwa katika mikoa TISA (9) Tanzania Bara yani Katavi, Rukwa, Dodoma, Singida, Mara, Simiyu, Pwani,Tanga na Kigoma. Mkoa wa Singida ni moja ya mkoa unaotekeleza mradi huu wa shule bora ,halmashauri zote saba(7) katika shule mbalimbali”.
Aidha Kanyambo alisema Mkutano huu umewashirikishawaandishi wa habari ili kushirikiana nao kutokana na umuhimu wao wa kuihabarisha jamii na jinsi yakuandika habari zinazohusu Elimu na chanagamoto zake na kufanya uhamasishaji wa jamii,wazazi umuhimu wa masuala ya elimu kwa Watoto.
“Tunahitaji ninyi waandishi wa habari mliopo kwenye halmashauri zote za wilaya kutuunga mkono katika kila jambo hili muhimu kwani sisi tunafanya kazi na vyombo vyote vya habari bila kuvibagua”.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.