- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Mh Rahabu Mwagisa amesisitiza kudumisha amani katika Kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 2020. Mh Rahabu ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wa uchaguzi wakiwemo Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, Viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine wakiwemo wakuu wa idara na wazee mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Wakati akifungua kikao hicho cha wadau mkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa nchi hiii inasifika kwa amani na utulivu, hivyo ni vyema kuendelea kuidumisha amani yetu bila kuruhusu kutumia siasa vibaya na kujikuta tunaiharibu. “Iwapo mtu ataona viashiria vya uvunjifu wa amani, milango iko wazi kufika na kuripoti ofisini kwangu ama kwenye vyombo vya ulinzi na usalamakwa haraka. Ni rai yangu pia kwa viongozi wa Dini mtuombee amani na uchaguzi uwe wa amani na utulivu. Ni wakati sasa wa kuhubiri amani kwa bidi zote na kuwahimiza wananchi kushiriki katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu” alisema Mh Rahabu.
Nae Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Manyoni Mashariki Ndg. Charles Edward Fussi amesema lengo la kikao hicho ni kuhabarishana juu ya ratiba nzima ya shughuli za uchaguzi ili kuweza kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli hizo ikiwemo kuwafahamisha wananchi juu ya nini kinaendelea kuhusiana na Uchaguzi mkuu ili wajue ratiba na waweze kushiriki pale wanapotakiwa kushiriki kama vile kujitokeza katika shughuli za kampeni zinazotarajia kuanza tarehe 26 mwezi huu ili kusikiliza sera za wagombea na pia kuwahamasisha pia wananchi kujitokeza siku ya kupiga kura katika vituo walivyojiandikisha ifikapo oktoba 28, mwaka 2020.
Wakichangia maoni yao, mmoja ya wadau wa kikao hicho Daudi Yina Silla ambaye anatoka Taasisi ya wasaidizi wa kisheria alisema, “Vyama vya siasa vitumie muda vizuri, na kila mwanasiasa afanye mambo ambayo hayatavunja sheria na haki za wengine. Ni ombi letu pia wazingatie kufanya siasa za heshima ambazo hazitatugawa wananchi kutoka katika amani na umoja tulionao”.
Katika uchaguzi wa jimbo la Manyoni Mashariki, wananchi wanatarajiwa kujitokeza katika kupiga kura hapo oktoba 28 ili kumchagua Rais, Mbunge na Madiwani.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.