- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waendesha Baiskeli Afrika Mashariki Watua Manyoni, Wapanda Miti kwa Ajili ya Mazingira
Manyoni, 26 Agosti 2025 – Halmashauri ya Manyoni imepokea kwa shangwe kundi la waendesha baiskeli kutoka nchi za Afrika Mashariki, ambao wako kwenye safari ya kipekee iliyoanzia Jijini Kampala, Uganda, wakiwa na ujumbe wa kulinda mazingira kwa kupanda miti katika shule mbalimbali za sekondari.
Katika kuendeleza dhamira yao ya kuhimiza uhifadhi wa mazingira, waendesha baiskeli hao walifika Shule ya Sekondari Mwanzi na kushirikiana na wanafunzi pamoja na walimu kupanda miti kadhaa kama alama ya urithi endelevu kwa vizazi vijavyo.
Safari hiyo ya baiskeli ina lengo la kuunganisha vijana wa Afrika Mashariki kupitia mazingira, afya na mshikamano wa kikanda, huku ikisisitiza mchango wa kila mmoja katika kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Wakazi wa Manyoni wameipokea ziara hiyo kwa furaha na kuahidi kuendeleza kampeni hiyo ya upandaji miti ili kulinda mazingira na kuboresha hali ya hewa kwa maendeleo ya taifa.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.