- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WAKULIMA WA CHIKUYU-MANYONI WAMPONGEZA RAISI SAMIA KWA MIRADI YA UMWAGILIAJI
Wakulima wa maeneo ya Chikuyu, Maweni na Kintinku Wilayani Manyoni,Singida wamempongeza Raisi Samia Suluhu Hassan na serikali ya awamu ya sita kupitia wizara ya kilimo kwa mikakati ya ujenzi wa miradi mipya ya umwagiliaji na ukarabati wa miradi ya zamani katika wilaya ya Manyoni.
Hayo yamesemwa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo Mh Anthony Mavunde katika miradi ya umwagiliaji Chikuyu,Ntambaliza,Ngaiti na Udimaa ambapo amepata nafasi ya kukagua skimu zote hizo zinazofanya kazi ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na kukuza uchumi wa wakulima.
"Mh Raisi Samia anayo dhamira kubwa ya kuona mkulima wa Tanzania ananufaika na kilimo chake kwa kulima kwa tija na kuongeza kipato kupitia kilimo cha uhakika cha umwagiliaji.
Mh Raisi ameelekeza eneo la Mbwasa ,manyoni kujengwa bwawa lenye thamani ya Tsh 20 bilioni lenye uwezo wa uhifadhi maji wa mita za ujazo milioni kumi pamoja na skimu za umwagiliaji katika eneo hilo.
Na mimi namuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji kusimamia ukarabati wa kingo za mto za mradi wa umwagiliaji Chikuyu sambamba na kufanya usanifu wa miradi ya Ntambaliza,Udimaa na Ngaiti ili kuwa na chanzo cha uhakika cha maji na miundombinu ya mifereji ya maji ya umwagiliaji" Alisema Mavunde
Akitoa ufafanuzi katika baadhi ya mambo yaliyojitokeza,Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Ndg. Raymond Mndolwa amesema kwamba Tume imejipanga kuhakikisha miradi yote mipya ya skimu ya umwagiliaji inakua na chanzo cha uhakika cha maji ili kuruhusu shughuli za kilimo cha umwagiliaji kufanyika zaidi ya mara moja kwa mwaka.
Naye Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mh. Dr. Pius Chaya kwa niaba ya wakulima wote amempongeza Raisi Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya kilimo kwa kazi kubwa ya miradi ya umwagiliaji inayofanyika katika wilaya ya Manyoniambapo kupitia miradi hiyo wananchi wa maeneo hayo watakuza vipato vyao na kutatua changamoto kubwa ya Ajira hususani kwa vijana
Mkuu wa Wilaya ya Iramba ambaye anakaimu wilaya ya Manyoni kwa sasa Mh. Suleiman Mwenda ameahidi kwa niaba ya serikali ya wilaya kusimamia utekelezaji wa miradi hii kwa uadilifu na umakini mkubwa ili kuleta matokeo chanya kwa wakulima wa mpunga wa skimu hizo.
Mh Naibu Waziri wa kilimo akisalmiana na wananchi
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.