- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Chama sasa kimeimarishwa sio kama zamani ,kila kanda ina ofisi ya Wakili wa TALGWU ili kusimamia kesi za wanachana wake na kutoa ushauri pia kwa wanachama juu ya mambo mbalimbali.Chama kipo kwaajili ya kulinda na kutetea maslahi ya wanachama wake nchi nzima kwa matawi yote hivyo wanachama jivunieni chama chenu.
Haya yamesemwa na Katibu Mkuu wa TALGWU Taifa Ndg. Rashid Mtima leo alipokua akihutubia mkutano wa wanachama wa TALGWU uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Wanachama wa Talgwu wakiwa tayari kuimba wimbo wao wa Chama
Pia Mtima alisema kuna madodoso mtapata wanachama wote muyatumie kujaza taarifa zenu zote ikiwemo madai na muyawasilishe kwenye matawi ili tukiwa tunajenga hoja tunakua na data ambazo tumezikusanya kutoka kwa wanachama wetu
Nasisitiza mikutano ifanyike kwenye matawi ili wanachama muongee na kujadili namna nzuri ya kukuza utendaji kazi kila mmoja kwa eneo lake pia kuimarisha chama
MSHIKAMANO: DAIMA
TALGWU :CHAMA IMARA ,HUDUMA BORA KWA WANACHAMA
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.