- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maelekezo haya yametolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano Mhe . Kundo A. Mathew Tarehe 16 Januari 2024 alipotembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa Mnara wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel uliojegwa kata ya Sasilo.
"Natoa maelekezo kwa Kampuni zote za mawasiliano Tanzania kutoa mikataba kwa wananchi wanaotoa maeneo yao ili kujenga minara na mikataba hiyo ipelekwe na kusainiwa mbele ya wakurugenzi wa Halmashauri ya eneo husika ili kuwashauri wananchi vizuri juu ya ubora wa mikataba hiyo"
Wananchi wa Sasilo hamna budi kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kuhakikisha mnapata huduma hii ya mawasiliano huku vijijini, lakini pia kipekee kumshukuru Mbunge wenu Dkt Pius Chaya kwa kuwasemea kwani haikua rahisi kupata mradi huu wa Mnara ila kwakua alikua analisemea kila siku kwa uzito mkubwa tukaona tuwape kwanza wananchi wa Sasilo.Alisema Mhe. Kundo
Mnara huu wa Kampuni ya Mawasiliano Airtel utasaidi kata ya Sasilo pamoja vijiji vyake lakini pia tutaendelea kuhakikisha kata na vijiji vingine ambavyo vina changamoto ya mtandao vinapata mtandao kama kata ya Sasilo mlivyopata.
Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe. Thomas Apson ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Alitoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Pamoja na Naibu waziri wa Mawasiliano kufika Wilaya ya Manyoni kukagua mradi huu na kujiridhisha kazi nzuri iliyofanyika, lakini pia alishukuru Serikali pamoja na wadau wa Mawasiliano Mtandao wa Airtel kujenga mnara huo ambao utawasaidia wananchi Wilayani Manyoni.
"Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan anaupiga Mwingi sana tunamshukuru sana yeye na Serikali yake kwani wananchi wa Manyoni Hususani kata hii ya Sasilo inaenda kunufaika na mnara huu, lakini pia niwashukuru wadau wetu wa mawasiliano Aitel kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha wananchi hawa wanapata mawasiliano.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.