- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa julai 15 , 2022,amekagua maendeleo ya ujenzi na kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Singida inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kata ya Solya
Akizungumza na wananchi wakati wa hafla ya uzinduzi huo Majaliwa amesema kuwa amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi huo na amepongeza uongozi wa Halmashauri pamoja Mhandisi anayesimamia ujenzi huo na kwamba ameongeza kuwa kukamilika kwa shule hiyo kutaenda kupumguza utoro na mimba kwa wanafunzi wakike
Katika hatua nyingine Mjaliwa amefanya kikao na watumishi wa Serikali na Taasisi za umma kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Rc Mission Itigi ambapo amewaagiza watumishi kufanya kazi kwa juhuhdi ili kuwa na matokeo na si kwa mazoea amesema kuwa eneo lenye usimamizi dhaifu daima haliwezi kuwa na maendeleo chanya na yenye tija
Majaliwa amesema kila Kiongozi anapaswa ahakikishe anatekeleza majukumu yake na kutoa taarifa kwa wananchi juu ya miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ili wananchi waweze kuelewa kile Serikali inafanya kwa ajili yao
Aidha Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Singida Mzalendo Widege kuwahoji wakusanya mapato katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Wilaya ya Manyoni na wakusnaya mapato wa minada pamoja na Mkuu wa kitengo cha tehama maagizo haya yamekuja baada ya kuwepo kwa udanganyifu katika ukusanyaji na uwasilishaji wa fedha zinazokusanywa.
Majaliwa amesema kuwa kuna wizi mkubwa wa mapato ya Serikali kupitia mifumo ya makusanyo kwenye Halmashauri mbalimbali hivyo ameagiza kila aliyepewa dhamana ya kusimamia kuhakikisha anasimamia kwa uweledi mkubwa ili fedha hizo zikusanywe na kuweza kufanya miradi ya maendeleo iliyopo katika Halmashauri na si vinginevyo.
“ndugu wananchi Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raisi Samia Suluhu Hassan iko makini na haina mzaa katika matumizi ya fedha za umma hivyo niwambie kabisa hakuna atakayebaki salama na wala hakuna mtumishi atakayeonewa kama atakiuka haya”alisisitiza Majaliwa
Katika ziara yake pia Majaliwa amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la wagongwa wa dhalula EMD linalojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni ambapo amemwagiza Mganga Mkuu kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati na kwa viwango kama ilivyoelekezwa ili wananchi waweze kupata huduma.
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.