- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Limeagiza kupitia kikao chake cha Baraza kilichofanyika tarehe 03 Novemba 2022 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni shule ambazo ni shule ambazo hazijasajiliwa zikaguliwe na Timu wa Udhibiti Ubora ili ziweze Kupata usajili,Baraza hilo limeagiza hayo kufanyika kwa Haraka ili mwaka mpya wa masomo unapoanza shule hizo ziwe zimesajiliwa na hii itasaidiwa shule hizo kupata stahiki zake kama shule zingine zinazojitegemea mfano walimu, miundombinu ya ufundishaji na fedha za kuendeshea shule hizo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Mh Jumanne Mlagaza alisema ndani ya huu muda mchache kabla ya mwaka mpya wa masomo kuanza shule zote za msingi na sekondari ambazo hazijasajiliwa zikakaguliwe na timu ya udhibiti ubora ili kwa zile ambazo zitakua zimekidhi vigezo zipate kusajiliwa ziwe shule rasmi.Sambamba na hili Serikali imetupatia fedha Bil 1.7 kwaajili ya ujenzi wa madarsa shule za sekondari hivyo kwa pamoja naomba tushirikiane ili kuhakikisha madarsa haya yanakamilika kwa wakati na tunakabidhi tarehe 03 Disemba 2022 kama tulivyokubaliana halmashauri ya Wilaya ya manyoni.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Ndg Fadhili Chimsala alikua na haya ya kusema kwenye hoja hii. "Zoezi la kutembelea na kufanya ukaguzi kwa shule hizi ambazo hazina usajili limeanza tayari na kwa maagizo ya Baraza nitahakikisha zoezi hili linakwenda haraka ili kufikia malengo hayo ya shule hizi kupata usajili kabla ya mwaka mpya wa masomo kuanza.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh Rahabu Mwagisa alisema, Kwa niaba ya wananchi wa manyoni tunaishukuru sana Serikali ya awamu ya Sita chini ya Raisi watu Nh Samia Suluhu Hassani kwa kutupatia fedha nyingi sana Wilaya ya Manyoni za maendeleo mbalimbali ikiwepo sekta ya Afya, Barabara,Elimu,Maji Umeme na miradi mingineyo ombi langu kwenu kwa pampoja tusimamie fedha hizo ili zitumike vizuri na miradi ukamilike kwa wakati na iwe yenye kulingana na thamani ya fedha zilizotumika.
Ni matumaini yangu kuwa Waheshimiwa Madiwani pamoja na Watendaji wote tunapokua kwenye majukumu yetu tunawaeleza wananchi namna Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Mama yetu Mh Samia Suluhu Hassani inavyofanya jitihada kuhakikisha wananchi wa Manyoni wanapata maendeleo kwa kutuleta fedha hizi nyingi za kutekeleza Miradi mbalimbali. Mh Mwagisa alisisitiza.
Mh Mwagisa alimalizia kwa kusema "Nimeanza ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kufanya mikutano ya hadhara ili kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua,katika ziara zangu ninaambatana na Wakuu wa divisheni na vitengo na wakuu wa taasisi zote zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ili kila mmoja aweze kutoa majibu ya kero za wananchi papo kwa papo.Nitaendelea kufanya ziara hizi kuzunguka kata zote ila niwaombe Waheshimiwa Madiwani kabla sijafika kwenye maeneo yenu endeleeni kufanya mikutano na kutatua kero za Wananchi kwenye Maeneo yenu.
Waheshimiwa Madiwani wakiendelea na Baraza
Baadhi ya wataalamu mbalimbali waliohudhuria baraza la madiwani
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.