- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wananchi Kintinku, Maweni na Makanda Wapewa Elimu ya Umiliki wa Ardhi – “Tuwe na Hati Miliki” Asema Afisa Ardhi
Manyoni – Katika kuhakikisha usalama wa mali na kupunguza migogoro ya ardhi kwa wananchi, Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Ndg. Mwakila Uswege, ametoa wito kwa wananchi wa Kata ya Kintinku, Maweni na Makanda kuhakikisha wanamiliki ardhi zao kwa hati halali.
Akizungumza tarehe 9 Oktoba 2025 katika Ofisi ya Kijiji cha Udimaa, katika wiki ya huduma za Ardhi, Ndg. Uswege alieleza kuwa umiliki rasmi wa ardhi kwa hati miliki ni hatua muhimu kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
> “Ukiwa na Hati Miliki ya Ardhi, una uhakika na usalama wa eneo lako, unakuwa na uwezo wa kulitumia kama dhamana ya kupata mikopo benki, na muhimu zaidi unapunguza migogoro ya ardhi na majirani zako,” alisema Uswege.
Katika mkutano huo uliowakutanisha wananchi kutoka kata zote tatu, elimu ya umiliki wa ardhi ilitolewa pamoja na kugawiwa hati miliki za kimila kwa baadhi ya wananchi waliokamilisha taratibu.
Afisa Mipango Miji, Ndg. Jonas Aniceth, naye alieleza hatua za msingi zinazopaswa kufuatwa ili kupata hati miliki ya ardhi, ikiwemo kujaza fomu za maombi, kufanya uhakiki wa eneo, upimaji wa kitaalamu na maandalizi ya nyaraka za umiliki.
Halmashauri ya Manyoni inaendelea na kampeni ya kuwafikia wananchi wote kupitia elimu ya umiliki sahihi wa ardhi ili kuwezesha maendeleo na utulivu katikaJamii.
@anastaziatutuba @drmashinjivincent @wizara_ya_ardhi @msemajimkuuwaserikali @maelezonews @singidars
HALMASHAURI YA WILAYA MANYONI
Sanduku la Posta: S.L.P 60 MANYONI
Simu: +255 26 2540136
Namba ya Simu: +255 26 2540136
Barua Pepe za Watumishi: ded.manyonidc@singida.go.tz, ded@manyonidc.go.tz
Haki Ya Kunakiri ©2019 Halmashauri Ya Wilaya Ya Manyoni . Haki Zote Zimehifadhiwa.